Zambia yaondoa wasiwasi wa upotezaji ajira kutokana na uhuishaji wa TAZARA

(CRI Online) Agosti 01, 2025

Serikali ya Zambia imepuuzilia mbali ripoti kwamba kuhuishwa kwa Mamlaka ya Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA) kutasababisha watu kupoteza ajira.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya Uchukuzi na Usafirishaji ya Zambia jana Alhamisi, imesema hakuna mfanyakazi atakayeachishwa kazi chini ya mpango wa uhuishaji wa mamlaka hiyo, aikibainisha kuwa wafanyakazi kati ya 200 na 300 watapita kwenye ajira yenye masharti nafuu, lakini wengi wao wataendelea kuwa na ajira.

Taarifa hiyo pia imesema vyama vya wafanyakazi ndani ya TAZARA vinafahamu kikamilifu na vimehusika katika mchakato mzima wa majadiliano, ili kuhakikisha kuwa hakuna mfanyakazi anayeachwa nyuma, na mabadiliko kwenye reli hiyo yanatarajiwa kuongeza mahitaji ya wafanyakazi, hasa katika kipindi cha miaka mitatu ya kwanza ya utekelezaji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha