IOM yaeleza wasiwasi kuhusu misukosuko ya tabianchi na wakimbizi nchini Somalia

(CRI Online) Agosti 01, 2025

Naibu mkurugenzi mkuu wa operesheni wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Bi. Ugochi Daniels, ameeleza wasiwasi kuhusu misukosuko ya tabianchi na wakimbizi inayoendelea nchini Somalia, baada ya kumaliza ziara ya siku nne nchini humo.

Bi. Ugochi Daniels amesema kupitia taarifa iliyotolewa Alhamisi mjini Mogadishu kuwa, watu wa Somalia wanakumbwa na athari mbaya zaidi za msukosuko wa tabianchi, ambazo zinasababisha wakimbizi wa ndani, shinikizo kwa miji na mivutano ya kugombea rasilimali zinazopungua siku hadi siku.

Kwa mujibu wa ofisa huyu, Wasomali wanakabiliwa na ukame usioisha, mafuriko na mivutano, ambavyo vimesababisha watu milioni 3.6 kukimbia makwao huku karibu nusu ya watu wote wa nchi hiyo wakiathiriwa na majanga yanayohusiana na tabianchi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha