Jumuiya ya Afrika Mashariki yasisitiza tena ahadi za soko la pamoja baada ya Tanzania kupiga marufuku wafanyabiashara ndogo wa kigeni

(CRI Online) Agosti 01, 2025

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imesisitiza tena dhamira yake kuendeleza mchakato wa mafungamano ya kikanda baada ya Tanzania kupiga marufuku wageni kuendesha biashara ndogo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa EAC Bi Veronica Nduva jana Alhamisi, nchi wanachama zinatakiwa kufuata itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya hiyo, ambayo inahimiza mjongeo huru wa bidhaa, huduma na watu katika kanda hiyo.

"Nchi wanachama lazima zijizue kurudisha nyuma au kuzuia sekta na biashara ambazo zilishazifanya kuwa huria" taarifa hiyo imesisitiza, ikirejelea Kiambata V cha ratiba ya ahadi ya mpango wa soko la pamoja la EAC kwa dhamira ya uhuria endelevu wa huduma.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, jumuiya ya EAC inahimiza nchi zote wanachama kutekeleza wajibu wao kimkataba ili kulinda ukamilifu wa soko moja la kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha