Rais wa China na mkewe wakutana na mfalme na malkia wa Cambodia

(CRI Online) Agosti 27, 2025

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China na mkewe Bi Peng Liyuan hapa Beijing wamekutana na mfalme wa Cambodia Norodom Sihamoni na mama malkia Norodom Monineath Sihanouk.

Rais Xi amekaribisha kwa ukarimu mfalme Sihamoni na mama malkia Monineath kufanya tena ziara nchini China, na kumkaribisha mfalme Sihamoni kushiriki kwenye shughuli ya maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa vita vya watu wa China kupambana na uvamizi wa Japani na ushindi wa vita vya dunia vya kupinga ufashisti. Rais Xi amesema, tangu mwezi wa Aprili mwaka huu alipofanya ziara nchini Cambodia, alipokelewa kwa ukarimu na kwa urafiki na mfalme na watu wa Cambodia, na kufurahia ziara yake. Uhusiano kati ya China na Cambodia umepitia mabadiliko ya hali ya jumuiya ya kimataifa, na kuunda urafiki imara, wenye thamani kwa watu wa nchi mbili, na ambao unastahili kuthaminiwa na pande mbili.

Mfalme Sihamoni na mama malkia Monineath wamesema, wanafurahi kuja tena China na kualikwa kushiriki kwenye shughuli ya maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa vita vya watu wa China kupambana na uvamizi wa Japan, watu wa China wametoa mchango mkubwa katika ulinzi wa amani ya dunia, ambao wanastahili kukumbukwa milele. Amesema wakati rais Xi akifanya ziara ya kihistoria nchini Cambodia, pande mbili zilikumbuka urafiki na kujadili ushirikiano, huku zikipata mafanikio mengi. Cambodia siku zote inachukulia uhusiano kati yake na China kuwa wa kimkakati, huku ikitaka kukuza uhusiano wa jadi na urafiki na kujenga jumuiya ya Cambodia na China yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha