Uwekaji wa nguzo za chuma kwenye Daraja la Mto Hanjiang la reli ya kasi ya Xi'an-Shiyan wakamilika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 19, 2025
Uwekaji wa nguzo za chuma kwenye Daraja la Mto Hanjiang la reli ya kasi ya Xi'an-Shiyan wakamilika
Picha iliyopigwa kwa droni Agosti 18, 2025 inaonyesha eneo la ujenzi wa daraja la Mto Hanjiang la reli ya kasi ya Xi'an-Shiyan katika mji wa Shiyan, Mkoani Hubei, China. (Xinhua/Cheng Min)

Uwekaji wa nguzo za chuma kwenye Daraja la Mto Hanjiang, ambalo ni mradi muhimu wa reli ya mwendo wa kasi ya Xi'an-Shiyan, umekamilika.

Ikiwa imepangwa kuwa na kasi ya kilomita 350 kwa saa, reli hiyo yenye urefu wa kilomita 255.76, inayounganisha mji wa Shiyan Mkoani Hubei na Xi'an, Mkoa wa jirani wa Shaanxi, inatarajiwa kufupisha muda wa kusafiri kati ya miji hiyo miwili hadi chini ya saa moja.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha