Rais Xi akutana na mkuu wa baraza la chini la Bunge la Russia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 27, 2025

Rais Xi Jinping wa China akutana na mwenyekiti wa baraza la chini la Bunge la Russia (Duma) Bw. Vyacheslav Volodin, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Agosti 26, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenyekiti wa baraza la chini la Bunge la Russia (Duma) Bw. Vyacheslav Volodin, mjini Beijing.

Kwenye mkutano wao Rais Xi amesema uhusiano kati ya China na Russia ni uhusiano ulio imara zaidi, uliokomaa na wenye umuhimu wa kimkakati kati ya nchi kubwa katika dunia ya leo yenye hali ya misukosuko na mabadiliko, na kwamba kuendelea kuhimiza maendeleo ya hali ya juu kati ya China na Russia kunalingana na maslahi ya kimsingi ya watu wa nchi hizo mbili na pia ni chanzo cha utulivu wa amani duniani.

“Mwezi Mei mwaka huu, nilifanya ziara ya kiserikali nchini Russia na kuhudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 80 ya ushindi wa Vita Vikuu vya Kulinda Nchi vya Umoja wa Kisovieti,” amesema Rais Xi, na kumwambia kuwa wiki ijayo China itafanya gwaride kubwa la kuadhimisha miaka 80 ya ushindi katika Vita vya watu wa China vya kupambana na uvamizi wa Japan na vita vya dunia vya kupinga ufashiti.

Amesema China na Umoja wa Kisovieti, zikiwa ni medani kuu za vita vya pili vya dunia barani Asia na Ulaya, mtawalia, zilitoa muhanga mkubwa wa kitaifa katika kupambana na uvamizi wa wajapani na Unazi wa Ujerumani, na zilichangia ushindi wa vita vya pili vya dunia.

Rais Xi pia amesema ni muhimu kwamba pande hizo mbili kuendeleza urafiki wa jadi, kuimarisha kuaminiana kimkakati, kuimarisha ushirikiano katika pande zote, na kulinda kwa pamoja usalama na maslahi yao ya maendeleo.

Ametoa wito kwa pande hizo mbili kuhimiza mshikamano na nchi nyingine za Kusini ya dunia, kujitolea kwa ajili ya mshikamano wa pande nyingi, na kuhimza utaratibu wa kimataifa wenye haki na usawa.

Bw. Volodin amemfikishia Rais Xi salamu kutoka kwa Rais Vladimir Putin wa Russia, na kusema chini ya uongozi wa kimkakati wa marais hao wawili, uhusiano kati ya Russia na China umepata maendeleo zaidi na kuzaa matunda.

Rais Xi Jinping wa China akutana na mwenyekiti wa baraza la chini la Bunge la Russia (Duma) Bw. Vyacheslav Volodin, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma  la Beijing, China, Agosti 26, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

Rais Xi Jinping wa China akutana na mwenyekiti wa baraza la chini la Bunge la Russia (Duma) Bw. Vyacheslav Volodin, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Agosti 26, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha