China yajenga mtandao mkubwa zaidi duniani wa kuchaji magari ya umeme

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 27, 2025

Beijing - China imejenga mtandao mkubwa zaidi duniani wa kuchaji magari ya umeme (EV) katika kipindi cha Mpango wa 14 wa Miaka Mitano (2021-2025).

Mkuu wa Idara ya Nishati ya Kitaifa ya China, Bw. Wang Hongzhi, amesema kwenye mkutano na wanahabari kwamba China pia imejenga mfumo wa nishati mbadala unaokua kwa kasi zaidi duniani, na sehemu ya nishati mbadala katika uwezo wake wa uzalishaji wa umeme uliowekwa imeongezeka kutoka karibu asilimia 40 hadi karibu asilimia 60.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha