Biashara kati ya China na Zambia yaimarika kufuatia utekelezaji wa sera ya kufuta ushuru

(CRI Online) Agosti 27, 2025

Balozi wa China nchini Zambia Han Jing amesema, utekelezaji wa ushuru sifuri umeimarisha kidhahiri biashara ya pande mbili kati ya China na Zambia.

Balozi Han amesema, thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili imefikia dola za kimarekani bilioni 3.56 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.5 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

Akizungumza katika Baraza la 8 la hafla ya Uzinduzi wa Ushirikiano wa Kampuni za China nchini Zambia (ACCZ) jumatatu wiki hii, Balozi Han amesema, kupandishwa ngazi ya uhusiano kuwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, kumeimarisha kuaminiana na kupata matokeo zaidi kutokana na ushirikiano huo.

Waziri wa Uchukuzi na Ugavi wa Zambia Frank Tayali amesifu kampuni za China kwa kuchukua nafasi kubwa katika kuchochea maendeleo ya uchumi ya Zambia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha