

Lugha Nyingine
Afrika yazindua mpango wa kuimarisha mwitikio wa mlipuko wa kipindupindu
Mpango wa kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana kwa ufanisi zaidi na milipuko ya kipindupindu umezinduliwa jana jumanne, huku wito ukitolewa kwa viongozi wa kitaifa kuchukua uwajibikaji katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Mpango wa Mwitikio wa Mlipuko wa Kipindupindu Afrika ulizinduliwa kando ya Mkutano wa 75 wa Kamati ya Kikanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani (WHO) uliofanyika mji mkuu wa Zambia, Lusaka, na unalenga kuzipatia nchi mwongozo wa mwitikio wa haraka na wa pamoja kwa magonjwa ya mlipuko.
Akizundua mpango huo, rais wa Zambia Hakainde Hichilema amewataka viongozi wa Afrika kuanzisha vikosi kazi vya rais kuhusu kipindupindu, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji wa ngazi ya juu na uratibu.
Kwa mujibu wa WHO, nchi 33 barani Afrika zimeripoti maambukizi ya kipindupindu mwaka 2024, huku zikiwa na jumla ya kesi 804,721 na vifo 5,805.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma