

Lugha Nyingine
Baraza la mawaziri nchini Sudan lafanya mkutano wa kwanza tangu kuanza kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe
Serikali ya Sudan imeitisha mkutano wake wa kwanza mjini Khartoum, tangu vita ya wenyewe kwa wenyewe ilipoanza katikati ya mwezi April mwaka 2023, huku majadiliano yakijikita katika kuzindua 'maridhiano jumuishi ya Sudan na Sudan yasiyomtenga yoyote,' ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuchochea ufufukaji wa kitaifa.
Mkutano huo ulioongozwa na Waziri Mkuu wa mpito Kamil Idris na kuhudhuriwa na wajumbe wote 22 wa baraza la mawaziri, pia ulizungumzia kuendeleza uhusiano wa kigeni kupitia diplomasia rasmi na za umma, na kufanya kazi kuelekea kutimiza amani nchini humo.
Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano huo, Waziri Mkuu Idris amefafanua vipaumbele vya serikali, ambavyo ni pamoja na ukarabati baada ya vita, ufufuaji wa uchumi, kuboresha usalama wa raia, kuunga mkono kurejea kwa hiari kwa watu waliokimbia makazi yao na wakimbizi, na kuboresha sekta za uzalishaji ili kuongeza pato la taifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma