Rais wa Jamhuri ya Kongo ahimiza mchakato wa utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing

(CRI Online) Agosti 27, 2025

Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso, amesema yuko tayari kutekeleza kikamilifu majukumu yake akiwa mwenyekiti mwenza wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), na kuhimiza utekelezaji wa matokeo yaliyopatikana katika mkutano wa Baraza hilo uliofanyika mwezi Septemba mwaka jana mjini Beijing.

Rais Sassou amesema hayo jumatatu wiki hii alipokutana na balozi wa China nchini humo Bw. An Qing. Pia amesema nchi yake inapenda kuimarisha mawasiliano ya kirafiki na China, na kuhimiza uhusiano kati yake na China, na kati ya Afrika na China kupata maendeleo makubwa zaidi.

Kwa upande wake Balozi An amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na Jamhuri ya Kongo kuimarisha urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili, kuongeza kuaminiana kisiasa, na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha