Rais wa Zanzibar apongeza kikosi cha madaktari wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 27, 2025
Rais wa Zanzibar apongeza kikosi cha madaktari wa China
Rais Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar (katikati mbele) kwenye picha ya pamoja baada ya kuwatunuku nishani kikosi cha 34 cha madaktari wa China na wataalamu wa mradi wa kudhibiti kichocho unaofadhiliwa na China, kwa utumishi uliotukuka katika kuboresha huduma za afya za Zanzibar, Agosti 25, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM -- Rais Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar amewatunuku nishani kikosi cha 34 cha madaktari wa China na wataalamu wa mradi wa kudhibiti kichocho unaofadhiliwa na China, kwa huduma yao iliyotukuka katika kuboresha huduma za afya Visiwani Zanzibar.

Akizungumza kwenye hafla ya kukamilisha utumishi wao, Rais Mwinyi ameishukuru serikali ya China kwa ushirikiano wa muda mrefu na Zanzibar, hususan katika sekta ya afya. Amekishukuru kikosi cha 34 cha madaktari wa China kwa kazi nzuri katika muda wote wa kuwepo kwake Zanzibar, kwa kuwatibu wagonjwa, kutoa mafunzo kwa wanafunzi, kutoa msaada wa vifaa na dawa, na huduma zinazohitajika kwa Wazanzibari.

Rais Mwinyi pia amekipongeza kikundi cha mradi wa kudhibiti ugonjwa wa kichocho kwa jitihada zake katika kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya maambukizi, na kuahidi utayari wa serikali ya Zanzibar kukaribisha kikosi cha 35 cha madaktari wa China na kikundi kinachofuata cha wataalamu wa mradi wa kudhibiti kichocho.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha