Shirika la Ndege la Kenya lapanga kurejesha huduma za baadhi ya ndege ili kuongeza mapato

(CRI Online) Agosti 27, 2025

Shirika la Ndege la Kenya limesema kurejesha uwezo wa huduma za ndege ni kitu muhimu cha kuongeza mapato.

Mkuu wa shirika hilo Bw. Allan Kilavuka amesema kwenye mkutano wa uwekezaji mjini Nairobi kuwa, ndege moja iliyosimamisha kazi ya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner imerejesha huduma mwezi Julai, na ndege nyingine mbili zinatarajiwa kurejesha huduma mwishoni mwa mwaka huu.

Bw.Kilavuka ameongeza kuwa shirika lake litaendelea kuweka msisitizo kwenye kudhamiria kurejesha uwezo wa ndege zote, kuhimiza kuboresha gharama ya uendeshaji, na kutimiza programu ya ukusanyaji fedha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha