

Lugha Nyingine
Waziri wa Ghana ahimiza uwekezaji ili kuondoa umaskini wa nishati barani Afrika
(CRI Online) Agosti 27, 2025
Waziri wa nishati na mpito wa kijani wa Ghana John Abdulai Jinapor ametoa wito wa uwekezaji wenye malengo katika nishati barani Afrika ili kuondoa umaskini wa nishati barani humo.
Bw. Jinapor amesema hayo katika Kongamano la mustakabali wa Nishati wa mwaka 2025, akiongeza kuwa hadi sasa bado kuna waafrika zaidi ya milioni 600 ambao hawana umeme na zaidi ya bilioni moja wanaotegemea mkaa kupikia, hivyo kuna haja kubwa ya uwekezaji wa haraka wa nishati barani Afrika.
Bw. Jinapor amesisitiza kuwa maendeleo ya baadaye ya Afrika yanategemea ukuaji wa viwanda, na kufanya usalama wa nishati kuwa muhimu. Amelitaka bara hilo kuhamasisha mifumo shindani na endelevu ya kifedha kwa sekta ya nishati.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma