Bandari ya Qingdao yapanua biashara na nchi za SCO kupitia njia 42 za usafirishaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 28, 2025
Bandari ya Qingdao yapanua biashara na nchi za SCO kupitia njia 42 za usafirishaji
Wafanyakazi wakitoa kamba kwenye meli ya mizigo iliyokuwa ikielekea India kwenye Bandari ya Qingdao, Mkoani Shandong mashariki mwa China, Agosti 26, 2025. (Xinhua/Li Ziheng)

Kwenye miaka ya hivi karibuni, Bandari ya Qingdao katika mkoa wa pwani wa Shandong mashariki mwa China imetumia eneo lake na nafasi yake muhimu ya Maeneo ya Vielelezo vya Ushirikiano wa Kiuchumi na Kibiashara wa China na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) ili kuwezesha ushirikiano wa kibiashara wa pande nyingi kati ya nchi za Jumuiya ya SCO.

Kiasi cha usafirishaji wa makontena kutoka kwenye bandari hiyo na kupita kwenye njia ya Asia ya Kati, Njia ya India na Pakistani, na njia ya reli na baharini inayounganisha Japan, Korea Kusini na nchi za Asia ya Kati zimeshuhudia ukuaji zaidi wa mwaka hadi mwaka. Hadi sasa, Bandari ya Qingdao imeunganishwa na njia 42 za baharini hadi katika nchi za jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai, na kuzifikia bandari 30 katika nchi hizi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha