

Lugha Nyingine
Rais wa China apongeza mafanikio makubwa katika maendeleo na ushirikiano wa SCO
Rais wa China Xi Jinping amesema, nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) zimepata mafanikio makubwa na ya kihistoria katika maendeleo na ushirikiano wa Jumuiya hiyo.
Rais Xi amesema hayo leo jumatatu wakati akihutubia Mkutano wa 25 wa Baraza la Wakuu wa Nchi wanachama wa SCO linalofanyika Tianjin, kaskazini mwa China. Rais Xi amesema, nchi hizo ni za kwanza kuanzisha mfumo wa kuaminiana wa kijeshi katika maeneo yao ya mpaka, zikibadili mipaka yao kuwa kifungo cha urafiki, kuaminiana na kushirikiana. Pia amesema, nchi hizo ni za kwanza kuchukua hatua za pande nyingi dhidi ya nguvu tatu za ugaidi, ufarakanishaji na msimamo mkali, na pia ni za kwanza kuzindua ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.
Rais Xi ameongeza kuwa, nchi hizo pia zilitangulia katika kukamilisha mkataba wa ushirikiano wa kirafiki wa ujirani mwema wa muda mrefu, kutangaza ahadi yao ya kuendeleza urafiki kizazi hadi kizazi na kujizuia kutoka mivutano. Aidha, rais Xi amesema nchi wanachama wa Jumuiya hiyo pia zimeongoza katika kutoa nadharia ya utawala wa dunia unaohusisha majadiliano ya kina na mchango wa pamoja kwa ajili ya kunufaishana, zikitekeleza juhudi halisi za kivitendo za pande nyingi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma