Uzoefu mdogo wa kujihisi urithi wa utamaduni usioshikika katika kituo cha wanahabari cha Mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai 2025 mjini Tianjin (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 01, 2025
Uzoefu mdogo wa kujihisi urithi wa utamaduni usioshikika katika kituo cha wanahabari cha Mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai 2025 mjini Tianjin
Wanahabari wakitengeneza picha za mwaka mpya za Yangliuqing kwenye kituo cha wanahabari cha Mkutano wa mwaka huu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) mjini Tianjin, China, Agosti 31, 2025. (Xinhua/Zhang Xiaoyu)

Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai wa mwaka 2025 unafanyika kuanzia Agosti 31 hadi Septemba 1 mjini Tianjin. Kituo cha wanahabari cha mkutano huo kimekuwa na eneo la uzoefu wa urithi wa kitamaduni usioshikika, kuwapa wanahabari fursa ya kujaribu ufundi wa sanaa za urithi wa utamaduni usioshikika kama vile picha za mwaka mpya za Yangliuqing zilizotokana na uchongaji wa picha kwenye vibao, sanamu za ufinyanzi wa udongo za Zhang na utengenezaji wa vyombo vya mbao vya rangi ya kung'arisha.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha