

Lugha Nyingine
Rais wa Uganda asema uwekezaji wa China unachochea mageuzi ya viwanda
![]() |
Rais Yoweri Museveni wa Uganda akizungumza baada ya uzinduzi wa viwanda vipya katika eneo la viwanda la China-Uganda mjini Mbale, Uganda, Agosti 29, 2025. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua) |
MBALE –Rais Yoweri Museveni wa Uganda alisema ijumaa iliyopita kuwa eneo la kiviwanda na viwanda vipya vinavyowekezwa na China vina nafasi muhimu katika kuleta mageuzi ya viwanda nchini Uganda. Rais Museveni amesema hayo wakati akitembelea eneo la viwanda la China-Uganda mjini Mbale.
Rais Museveni, ambaye katika ziara hiyo alizindua viwanda vinne vipya vilivyowekezwa na China, na kuweka mawe ya msingi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vingine tisa, alisema ujenzi wa viwanda ni moja ya nguzo muhimu ambazo serikali inazipa kipaumbele ili kuwezesha maendeleo ya nchi. Amesema, "viwanda ni jibu kwa Uganda na kwa Afrika... Asanteni sana kwa kutusaidia kubadilisha nchi yetu."
Mji wa Mbale, liliko eneo hilo la viwanda uko kwenye njia kuu ya usafiri kutoka Uganda hadi bandari ya Mombasa katika nchi jirani ya Kenya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma