China yafanya tamasha kubwa la utamaduni kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Ushindi (2)

(CRI Online) Septemba 04, 2025
China yafanya tamasha kubwa la utamaduni kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Ushindi
(Picha/Xinhua)

Watu wapatao elfu sita jana Jumatano jioni walitazama tamasha kubwa la utamaduni lililofanyika kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 80 tangu kupatikana Ushindi wa Vita vya Watu wa China wa Kupambana dhidi ya Uvamizi wa Wajapan na Ushindi wa Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti.

Viongozi wa Chama na serikali Xi Jinping, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi, na Han Zheng, walihudhuria tamasha hilo lililofanyika katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Kabla ya tamasha hilo kuanza, Rais Xi na viongozi wengine walisalimiana na askari wastaafu waliopigana katika vita hivyo.

Chini ya kaulimbiu “Haki Imeshinda”, tamasha hilo liliangazia historia ya Vita vya Watu wa China vya Kupambana dhidi ya Uvamizi wa Japan na Vita ya Dunia vya Kupinga Ufashisti, kuonyesha jukumu la Chama cha Kikomunisti cha China kama nguzo ya mapambano hayo, na kuonesha roho isiyoshindwa ya taifa la China linaposimama kidete na mataifa yote duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha