Shindano la kiteknolojia linalofadhiliwa na mashirika ya China lahamasisha vijana wa Afrika kutafuta ubora (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 04, 2025
Shindano la kiteknolojia linalofadhiliwa na mashirika ya China lahamasisha vijana wa Afrika kutafuta ubora
Li Qingtang, mkuu mtendaji wa Kampuni ya AVIC International ya China, akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Msimu wa 10 wa Shindano ya Kiteknolojia la Afrika, Africa Tech Challenge (ATC) jijini Nairobi, Kenya, Septemba 1, 2025. (Xinhua/Li Yahui)

NAIROBI - Wakati Victor Njung'e mwenye umri wa miaka 23 alipopitishwa kushiriki Shindano la Kiteknolojia la Afrika, Africa Tech Challenge (ATC), Msimu wa 10, alifikiri kushinda tuzo ya juu ilikuwa ndoto tu. Lakini kupitia ujasiri na kudhamiria, mwanafunzi huyo wa uhandisi wa ufundi katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Kenya amewashinda mamia ya washindani katika shindano hilo lililochukua mwezi mzima, akijinyakulia nafasi miongoni mwa washindi wa juu katika kipengele cha washindani binafsi.

Katika hafla kuu ya ufunguzi wa shindano hilo jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, Jumatatu jioni, Njung'e alipokea shangwe za wenzake alipokuwa akielekea jukwaani kupokea tuzo yake.

"Nimepotewa kidogo maneno kwa sababu sikutarajia ushindi huu. Shindano hili la kiteknolojia, vyote kinadharia na kivitendo, lilikuwa gumu sana, lakini kupitia kudhamiria na kazi ya pamoja katika kundi, tumefanikiwa." amesema.

Ni mara yake ya kwanza kushiriki katika ATC, programu iliyozinduliwa mwaka 2014 ili kuimarisha ujuzi wa kiufundi na ustadi miongoni mwa vijana wa Afrika na kuwatayarisha kwa kazi za siku za baadaye.

Msimu huo wa 10, ulioanza Julai 28 hadi Agosti 29, ulileta pamoja timu 142 na washiriki 568 kutoka nchi 12 za Afrika. Washindani walijaribu ujuzi wao katika vipengele vitatu: uundaji wa programu za simu janja, uhandisi wa mitambo na udhibiti wa numerali wa kompyuta (CNC).

Njung'e, ambaye anajikita kusoma viwanda vya kutengeneza bidhaa, amesema amepata ujuzi mpya wa kubuni kwa kutumia kompyuta wakati huohuo pia akijifunza kazi ya pamoja katika kundi na kujenga urafiki wa kuvuka mipaka.

Kwa mshiriki wa Ghana Nuseno Alfred, mwenye umri wa miaka 23, kutajwa miongoni mwa washindi sita wa kipengele cha washindani binafsi kulikuwa kwenye manufaa sawa.

"Mafunzo haya yamekuwa mazuri tangu siku ya kwanza. Yote yalihusu usahihi, kupanua upeo wangu, na kunipa uzoefu wa soko la ajira." Nuseno amesema, akiongeza kuwa amenoa ujuzi wake katika CNC, kutengeneza programu za mashine na uchoraji kiufundi.

Hafla hiyo, iliyohudhuriwa na maafisa wakuu wa serikali, wanadiplomasia, na watendaji wa tasnia, imeandaliwa kwa pamoja na kampuni ya AVIC Innovation Holding ya China (AVIC INNO), Wizara ya Elimu ya Kenya, na Jumuiya ya Elimu ya China kwa mawasiliano ya Kimataifa.

Julius Ogamba, waziri wa elimu wa Kenya, amesifu mpango huo wa kuwapa vijana wa Afrika zana za kustawi katika zama ya kidijitali.

"Kupitia ATC, tunahakikisha kuwa vijana wa Afrika wanakuwa nguvu ya kuendesha Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, kusukuma vikomo na kutafuta ubora." Ogamba amesema, akiongeza kuwa mpango huo unawiana na Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika, ambayo inalenga kujenga nguvu kazi shindani, yenye ujuzi na vumbuzi duniani.

Hafla hiyo pia ilishuhudia kuzinduliwa kwa Ripoti ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Uwajibikaji Kijamii kwa ATC Nje ya Nchi, ikiangazia jukumu la programu hiyo katika kuzidisha kwa kina ushirikiano kati ya China na Afrika katika mafunzo ya ufundi stadi.

Li Qingtang, makamu mkuu mtendaji wa AVIC, amesema shirika hilo limeweka kipaumbele kwa maendeleo ya ujuzi wa kiufundi kwa vijana wa Afrika, kulingana na maadili yake ya uwajibikaji kwa kijamii.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha