Rais Macron asema nchi 26 zimeahidi kwa maendeleo ya usimamishaji vita nchini Ukraine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 05, 2025
Rais Macron asema nchi 26 zimeahidi kwa maendeleo ya usimamishaji vita nchini Ukraine
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa (kulia) akimkaribisha Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine wakati akiwasili kuhudhuria mkutano wa "Muungano wa Walio wa Hiariw" katika Ikulu ya Elysee mjini Paris, Ufaransa, Septemba 4, 2025. (Xinhua/Gao Jing)

PARIS - Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ametangaza jana Alhamisi kuwa nchi 26, nyingi zikiwa za Ulaya, zimeahidi rasmi kupeleka wanajeshi kama sehemu ya usimamishaji vita wa baadaye kati ya Russia na Ukraine, ingawa si moja kwa moja kwenye mstari wa mbele.

Akizungumza pamoja na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine kwenye mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano wa "Muungano wa Walio wa Hiari," uliofanyika katika Ikulu ya Elysee jijini Parisi, Macron amesema nchi hizo zitaunda "kikosi cha uhakikisho" ambacho kinaweza kupeleka wanajeshi nchini Ukraine au kutoa uungaji mkono ardhini, baharini na angani.

Ameongeza kuwa, baada ya mkutano huo, washiriki walifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Donald Trump wa Marekani na Marekani inatarajiwa kukamilisha mchango wake kwa uhakikisho wa usalama katika siku zijazo.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Rais Zelensky amekaribisha tangazo hilo akilielezea kuwa hatua "halisi" kwenda mbele na kusisitiza kwamba mkutano na Rais Vladimir Putin wa Russia, iwe wa pande mbili au wa pande tatu, "ni muhimu" kwa ajili ya kusukuma mbele juhudi za amani.

Tangazo hilo limefuatia mkutano wa mtandaoni wa muungano huo siku ya Alhamisi, ulioongozwa na Rias Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer. Kundi hilo, ambalo limeleta pamoja nchi karibu 30, nyingi zikiwa za Ulaya, limeahidi kutoa uhakikisho wa usalama kwa Ukraine.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha