Mji wa Wuxi wa China wajenga kwa hamasa uchumi wa kufungua mlango (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2025
Mji wa Wuxi wa China wajenga kwa hamasa uchumi wa kufungua mlango
Picha ikionesha mstari wa uzalishaji wa YADEA kwenye eneo la viwanda vya skuta za umeme huko Wuxi, Mkoa wa Jiangsu Mashariki mwa China Septemba 16, 2025. (Xinhua/Liu Jiaqi)

Mji wa Wuxi umefanya juhudi za kujenga uchumi wa kufungua mlango katika miaka ya hivi karibuni. Idadi ya viwanda na kampuni vinavyofanya biashara halisi ya uuzaji nje na uagizaji bidhaa imezidi 13,000, huku thamani ya biashara hizo ya mwaka ikizidi dola bilioni 100 za Kimarekani katika miaka minne iliyopita.

Katika miezi minane ya kwanza ya mwaka 2025, thamani ya jumla ya biashara ya uuzaji nje na uagizaji bidhaa ya mji huo imeweka rekodi mpya ya juu ya Yuan bilioni 535.34 (takriban bilioni 75.36 za Kimarekani), ambayo imeongezeka kwa asilimia 7.2 kuliko kipindi kama hicho mwaka uliopita.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Renato Lu)

Picha