Lugha Nyingine
Kundi la Nishati la Shenzhen, China lawa kinara katika kutekeleza mpango “Mji wa Taka-Sifuri” (4)
![]() |
| Picha ikionesha kambi ya watoto ya majira ya joto ya masomo ya mambo ya mazingira katika Bustani ya Kiikolojia ya Nishati ya Nanshan. (Picha/Kundi la Kampuni za Nishati la Shenzhen) |
Bustani ya Kiikolojia ya Nishati ya Nanshan ambayo ni mchangiaji mkuu wa ulinzi wa mazingira ndani ya Eneo Maalum la Kiuchumi la Shenzhen katika Mkoa wa Guangdong, China, huchakata tani 2,300 za taka za nyumbani kwa siku, ikifanikisha ushughulikiaji kamili wa taka zote za nyumbani katika Eneo la Nanshan hivyo kutekeleza mpango wa "Mji wa Taka-Sifuri."
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari wa Timu ya Utafiti Kuhusu Shenzhen ya People's Daily Online jana Alhamisi na Kundi la Kampuni la Nishati la Nanshan linaloendesha bustani hiyo, hadi kufikia Julai 2025, takriban tani milioni 10.01 za taka za nyumbani zilikuwa zimeshachakatwa kwa jumla.
Kundi hilo limeeleza kuwa, kwa kipimo cha kuwekwa kwenye uwanja wa kawaida wa soka, kiasi hicho kinaweza kufikia urefu wa mita takriban 981.
Kwa mujibu wa maelezo ya kundi hilo, uzalishaji wa jumla wa umeme kwa kutumia taka ulifikia takriban kilowati bilioni 4.2 za saa (kWh), zinazotosha kusambaza umeme kwa kaya milioni 17.5 kwa mwaka mzima, kulingana na wastani wa matumizi ya mwaka ya kilowati 2,759, ikiiingiza msukumo mkubwa katika maendeleo ya kijani ya mji wa Shenzhen.
Kutokana na mafanikio hayo, kundi hilo limeeleza kuwa, takriban tani milioni 1.37 za makaa ya mawe ya kawaida zimeokolewa, ikiwa ni sawa na kupunguza tani karibu milioni 3.7 za utoaji wa hewa ya kaboni.
"Hatua hii halisi inachangia nguvu thabiti katika utekelezaji wa malengo pacha ya China ya kufikia kilele cha utoaji wa kaboni na usawazishaji wa kaboni na vilevile uboreshaji wa mazingira ya ikolojia" imesema kundi hilo katika taarifa yake hiyo.
Aidha imeongeza kuwa, bustani hiyo imekadiriwa kuwa kituo cha kiwango cha AAA katika mfumo wa China wa kutathmini ushughulikiaji taka usio na madhara kwa mitambo ya kuchakata taka, ikitoa mchango mkubwa kwa mpango wa "Mji wa Taka-Sifuri" wa Eneo Maalum la Kiuchumi la Shenzhen.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




