Lugha Nyingine
Wachina wafanya shughuli ya kumbukumbu za vita dhidi ya uvamizi wa Japan, kutokana na matumaini yao kwa amani (3)
![]() |
| Watu wakitembelea kwenye Jumba la ukumbusho wa Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan mjini Beijing, China, Septemba 18, 2025. (Xinhua/Zhang Chenlin) |
SHENYANG — Honi za magari na kengele zilipiga sauti katika miji ya China Alhamisi asubuhi, ikiashiria kumbukumbu za miaka 94 ya Tukio la Septemba 18, lililokuwa siku ya kuanza Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan.
Mamia ya watu, wakiwemo askari wastaafu na jamaa zao, walikusanyika kwenye uwanja wa umma wa Jumba la Makumbusho ya Historia ya 9.18 huko Shenyang, mji mkuu wa Mkoa wa Liaoning kaskazini mashariki mwa China, ili kuwaomboleza watu waliopigana vita na kujitolea mihanga katika vita hivyo vya kupambana na uvamizi.
Saa 3 na dakika 18 asubuhi, wajumbe 14 kutoka sekta mbalimbali waligonga kengele kubwa kwa mara 14, ikiashiria miaka 14 ya mapambano magumu dhidi ya wavamizi wa Japan.
Katika mji mzima, sauti za honi ya tahadhari ya shambulizi la upigaji mabomu kutoka angani na honi za magari zilisikika kwa dakika tatu, huku watembea kwa miguu mitaani wakisimama kimya kwa kutoa heshima. Jumla ya skrini 118 za kielektroniki za nje, skrini 1,800 za mabasi na maelfu ya skrini za teksi zilionesha maandishi ya “kukumbuka historia na kuwaomboleza mashujaa.”
Tokea mwaka 1995, mji wa Shenyang umekuwa ukikumbuka tukio hilo kwa namna hii, na kuanzia mwaka 1995, mji huo unafuata desturi ya kutoa honi ya tahadhari ya shambulizi ya upigaji mabomu kutoka angani kila mwaka kwa kumbukumbu za Tukio la Septemba 18 la mwaka 1931. Katika siku hiyo ya mwaka huo, jeshi la Japan lilibomoa sehemu ya reli iliyoko karibu na Shenyang ambayo ilikuwa chini ya udhibiti wa jeshi la Japan, lakini jeshi la Japan lililaumu jeshi la China kuharibu reli kama kisingizio cha kuanzisha uvamizi. Usiku huo huo, jeshi la Japan lilipiga mabomu dhidi ya kambi za jeshi la China zilizo karibu na reli.
Baada ya tukio hilo, juhudi za mapambano za Wachina zimekuwa alama ya kuanzishwa kwa Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan, na pia Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, alisema Fan Lihong, mkuu wa Jumba la Makumbusho ya Historia ya 9.18, lililojengwa karibu na eneo la kutokea mlipuko wa mabomu.
Mwaka huu unaadhimisha miaka 80 tangu ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan, na katika vita hivyo Wachina waliofariki dunia au kujeruhiwa walifikia milioni 35.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




