

Lugha Nyingine
Kenya yazindua huduma ya reli ya mjini kupunguza msongamano katika Mombasa (7)
![]() |
Rais William Ruto wa Kenya akihutubia hafla ya uzinduzi wa huduma ya reli ya mjini ya Mombasa katika Kituo cha Reli cha Mombasa, Kenya, Septemba 17, 2025. (Xinhua/Yang Guang) |
MOMBASA — Rais wa Kenya William Ruto Jumatano alizindua huduma ya reli ya mjini ya Mombasa itakayounganisha maeneo ya kiini cha mji huo na kituo cha Reli ya Kisasa (SGR), ili kuboresha uwezo wa usafirishaji wa abiria na mizigo.
Maofisa waandamizi wa serikali, viongozi wa viwanda na viongozi wa eneo hilo walihudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi huo unaounganisha kituo cha SGR cha Miritini, kilichoko kaskazini-magharibi ya Mombasa, na eneo la kiini la biashara la mji huo.
Ujenzi wa mradi huo, uliofanywa na Shirika la Barabara na Madaraja la China (CRBC) kuanzia Agosti 2022, ulihusisha pia kilomita 16.8 za reli ya upana wa mita, ambayo baadhi ya sehemu yake ilijengwa na wakoloni wa Uingereza zaidi ya karne moja iliyopita.
Wakati wa ujenzi, CRBC ilijenga njia mpya za reli za kilomita 2.9, na kukarabati kilomita 13.9 za reli ya zamani ya upana wa mita.
Ruto alisifu sana ujenzi wa mradi huo wa kampuni ya China, akisema ujenzi huo umetoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu ya Kenya na ustawi wa umma, na utasaidia Mombasa kuwa lango la biashara na shughuli za kiuchumi katika Afrika Mashariki.
Mbali na kuimarisha uunganishaji wa maili ya mwisho kwa abiria wanaotumia huduma ya reli ya Mombasa-Nairobi SGR, inayojulikana kama Madaraka Express, huduma hiyo ya reli pia itawahudumia abiria wa kando za njia hiyo ya reli, na nauli ya tiketi ni ya shilingi 50 za Kenya, Ruto alisema.
Bw. Wang Lijun, meneja mkuu wa CRBC amesema, ujenzi wa mradi huo umeleta nafasi za ajira takribani 800 kwa watu wa eneo hilo, huku wafanyakazi wenyeji wakichukua zaidi ya asilimia 90 ya nguvukazi, ambapo wameongeza ujuzi na ufundi katika kazi zao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma