Xuzhou, China: Ambako haiba ya Enzi ya Han inakutana na mitindo ya kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 22, 2025

Jioni huleta mchanganyiko wa mandhari na sauti kwenye mitaa yenye pilika nyingi ya Xuzhou katika Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. Harufu ya supu ya kondoo na muziki wa Opera ya Liuqin huchanganyikana na vyakula vya mitaani vinavyotoa watu mate na shangwe kutoka kwa michezo ya soka la ridhaa.

Awali ukiwa ulijulikana kwa jina la Pengcheng, mji huo unaunganisha ustaarabu wa miaka 5,000 na uvumbuzi wa teknolojia mpya za hali ya juu.

Vitu vya Urithi wa kitamaduni wa kale vinadumisha

Xuzhou inashikilia nafasi ya pekee katika historia ya China ikiwa ni mahali pa kuzaliwa kwa utamaduni wa watu wa Kabila la Wahan, ikiwa na historia zaidi ya miaka 2,600 iliyorekodiwa ya maendeleo ya miji.

Vitu vya udongo vikionyeshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Xuzhou, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Agosti 2, 2025. (People's Daily Online/Su Yingxiang)

Vitu vya udongo vikionyeshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Xuzhou, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Agosti 2, 2025. (People's Daily Online/Su Yingxiang)

Pamoja nayo, sanamu za mashujaa wa terracotta, kuanzia askari hadi wacheza ngoma, huwapa watembeleaji mtazamo wa maisha ya kila siku ya kale.

"Sanamu hizi zinajumuisha urembo wa kuvutia wa sanaa ya Enzi ya Han. Kupitia mistari safi na ufundi wa kibobezi, mafundi wa kale walinasa vyote mila za kijamii na hamu ya kisanii ya wakati wao" anaeleza muongoza watembeleaji wa makumbusho hayo Zhang Yizhi.

Huanglou (Mnara wa Njano), moja ya alama za kitamaduni za mjini za Xuzhou, ukionekana Agosti 1, 2025. (People's Daily Online/Yu Le)

Huanglou (Mnara wa Njano), moja ya alama za kitamaduni za mjini za Xuzhou, ukionekana Agosti 1, 2025. (People's Daily Online/Yu Le)

Ili kuheshimu na kuhuisha urithi huu, mji huo umezindua mradi wa "Pengcheng Qili", njia ya kitamaduni yenye kilomita 3.5 inayounganisha miundombinu alama muhimu ya kihistoria. Mpango huu umeibua maisha mapya katika mitaa na majengo ya kale, ikiunda eneo la kitamaduni ambapo vitu vya urithi wa kitamaduni na biashara zinaishi kwa mapatano. Mapigo ya kitamaduni ya Xuzhou yanahisiwa si tu katika maeneo yake ya kihistoria lakini pia katika jadi zake zinazoishi.

Supu ya kondoo wa mtindo wa Xuzhou ikionekana Agosti 1, 2025. (People's Daily Online/Su Yingxiang)

Supu ya kondoo wa mtindo wa Xuzhou ikionekana Agosti 1, 2025. (People's Daily Online/Su Yingxiang)

Kila majira ya joto, Xuzhou hufanya Tamasha la Fuyang, ambapo wenyeji hukusanyika ili kufurahia supu ya kondoo kufuatia hekima ya kale ya "kupambana na joto kwa joto." Jadi hii, ambayo kwa sasa ni urithi wa kitamaduni usioshikika wa kitaifa wa China, inabaki kuwa tukio la kijamii linalothaminiwa la kuunganisha mji huo na siku zake za nyuma.

Mtalii kutoka Hispania Alvaro Lago alikuwa na shaka kuhusu supu ya moto katika joto la kuvuja jasho. Baada ya kuonja kwake kwa mara ya kwanza, mtazamo wake ulibadilika. "Wakati nikiwa nimemaliza hii, nitakuwa natokwa jasho mwili mzima... naipenda," alisema akiungana na wenyeji katika sherehe hiyo.

Mtalii kutoka Hispania Alvaro Lago (wa kwanza kutoka kushoto) akijaribu Opera ya Liuqin mjini Xuzhou, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Agosti 4, 2025. (People's Daily Online/Su Yingxiang)

Mtalii kutoka Hispania Alvaro Lago (wa kwanza kutoka kushoto) akijaribu Opera ya Liuqin mjini Xuzhou, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Agosti 4, 2025. (People's Daily Online/Su Yingxiang)

Urithi wa kitamaduni wa Xuzhou unapanuka hadi kwenye Opera ya Liuqin, aina ya sanaa ya kimkoa inayojulikana kwa mipangilio ya sauti za kusisimua nafsi. Ikichezwa kwa gitaa mahsusi lenye umbo la jani la willow, opera hiyo ya kiasili inaonyesha maisha ya kila siku mjini.

Licha ya kizuizi cha lugha, Alvaro alijikuta akivutiwa na maonyesho ya kujieleza ya Opera ya Liuqin. "Hisia ni kwa kila mtu duniani," alieleza baada ya kutazama onyesho moja la kijadi. "Licha ya vizuizi vya tamaduni na lugha, niliweza kuhisi furaha na ucheshi katika opera."

"Opera ya Liuqin inajumuisha utamaduni wetu wa kienyeji," anasema Yang Cheng, naibu mkurugenzi wa Kikundi cha Opera ya Liuqin cha Jiangsu. "Mtindo wake wa moyo mwepesi, wa ucheshi unaonyesha kikamilifu tabia ukarimu na wema wa watu wa Xuzhou."

Kituo cha kisasa cha uvumbuzi

Xuzhou ya kisasa imepata kutambuliwa kuwa "Mji Mkuu wa China wa Mitambo ya Ujenzi," huku kampuni ongozi ya sekta hiyo ya Xuzhou Construction Machinery (XCMG) ikionyesha umahiri wa kiteknolojia wa mji huo.

Malori ya kiotomatiki yanayotumia umeme ya kuchimba madini yakionekana yakifanya kazi kwenye mgodi wa wazi wa Yimin, Mkoa wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China. (Picha imetolewa kwa People's Daily Online)

Malori ya kiotomatiki yanayotumia umeme ya kuchimba madini yakionekana yakifanya kazi kwenye mgodi wa wazi wa Yimin, Mkoa wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China. (Picha imetolewa kwa People's Daily Online)

Kundi la Malori 100 ya kiotomatiki yanayotumia umeme ya kuchimba madini yaliyoundwa na kampuni ya XCMG na washirika wake yameanza kutumika kwenye mgodi wa wazi katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China, ikiwa ni matumizi makubwa zaidi ya magari hayo duniani kote.

"Yakiunganisha teknolojia za kujiendesha kiotomatiki, mawasiliano ya 5G, na nishati ya jua, magari haya hufikia asilimia 120 ya ufanisi wa uendeshaji wa binadamu huku yakiokoa tani 15,000 za mafuta kwa mwaka."

Uvumvuzi mwingine wa XCMG, "Steel Mantis", mashine ya kuchimba inayotembea, ambayo ni maarufu kwa kuonekana kwake katika filamu ya "The Wandering Earth 2," inaonyesha uwezo wa ajabu katika operesheni ya uokoaji ngumu ya majanga.

Moyo wa jumuiya katika vitendo

Ligi ya Soka ya Miji ya mkoa wa Jiangsu 2025, inayojulikana kwa jina la "Su Chao," iliyozinduliwa Mei, imechochea shauku ya mji mzima ya soka la mitaani. Ikiwa na mechi 60 katika raundi 10, ligi hiyo ya wachezaji wasio wataaluma imevutia wastani wa watazamaji 25,000 kwa kila mchezo, na ikivutia watu zaidi ya bilioni 1.3 kutazama mtandaoni.

Mechi ya soka katika Kituo cha Michezo cha Olimpiki cha Xuzhou Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Agosti 2, 2025. (People's Daily Online/Yu Le)

Mechi ya soka katika Kituo cha Michezo cha Olimpiki cha Xuzhou Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Agosti 2, 2025. (People's Daily Online/Yu Le)

Su Chao hukaribisha wachezaji kutoka hali zote, tofauti na ligi za kitaaluma. Wanafunzi, wafanyakazi wa kusambaza mizigo, watayarishaji programu na walinzi hushindana pamoja katika ligi hiyo, ikiakisi hali ya ujumuishi wa michezo ya jamii.

"Ikilinganishwa na ligi za kitaaluma, Su Chao iko karibu zaidi na watu wa kawaida," anasema mchezaji wa timu ya Xuzhou Li Guangpeng, ambaye anafanya kazi katika kampuni ya ulinzi. "Inaleta wachezaji na mashabiki karibu zaidi."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha