Lugha Nyingine
Wapiganaji 34 wauawa kwenye operesheni zilizofanywa na jeshi la Niger
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Niger vimetangaza kuwaua wapiganaji 34 kwenye operesheni mbili zilizofanywa katika kipindi cha wiki iliyopita kwenye maeneo ya magharibi ya nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo jana Jumapili inasema kuwa, operesheni ya kwanza ilifanyika Jumatano kwenye eneo la Dosso, wakati askari wa doria kutoka mji wa Soukoukoutane waliposhambuliwa na wapiganaji wapatao 50 wenye silaha wakiwa kwenye pikipiki.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Jeshi lilifanikiwa kuua wapiganaji 22 na kujeruhi wengine wengi, huku washambuliaji waliobaki wakikimbia kuelekea mpaka wa Mali. Aidha, imeeleza kuwa, askari wake saba wameuawa na wawili wengine kujeruhiwa.
Aidha, imeeleza kuwa, operesheni ya pili ilifanyika Ijumaa kwa mashambulizi ya angani na ardhini dhidi ya magaidi waliokuwa na pikipiki wakisafirisha mifugo ya wizi, na kuua magaidi 12.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



