Lugha Nyingine
Bingu Mutharika aongoza katika uchaguzi mkuu wa Malawi akifuatiwa na Rais wa sasa Chakwera
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi, duru ya pili ya matokeo rasmi yasiyo kamili kutoka kwenye uchaguzi mkuu wa Malawi uliofanyika Septemba 16 inaonesha kuwa rais wa zamani Peter Mutharika anaongoza, akifuatiwa na Rais wa sasa Lazarus Chawera, huku aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo Dalitso Kabambe akichukua nafasi ya tatu.
Kwa mujibu wa matokeo rasmi kutoka maeneo tisa yaliyotangazwa Ijumaa na Jumamosi na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi Jaji Annabel Mtalimanja, Bw. Mutharika alikuwa amepata kura 203,440, huku Chakwera akiwa na 153,507, ambapo zoezi la kuhesabu na uhakiki wa kura bado lilikuwa likiendelea katika Kituo cha kuhesabia kura cha Taifa mjini Lilongwe.
Mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi Jaji Mtalimanja ameuhakikishia umma kuwa matokeo ya urais yatatangazwa ndani ya siku nane kuanzia siku ya upigaji kura, kama inavyotakiwa na sheria za nchi hiyo. Pia ametoa wito kwa vyama vya kisiasa, wagombea, wafuasi wao na wadau kudumisha amani na utulivu wanaposubiri matokeo rasmi ya mwisho.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



