Lugha Nyingine
Jumuiya za Wachina zatoa msaada wa mahitaji kwa waathiriwa wa mgogoro katika Mkoa wa Savannah, Ghana

Wakazi walioathiriwa na mgogoro wakichukua msaada wa mahitaji uliotolewa na jumuiya za Wachina nchini Ghana katika Mkoa wa Savannah, Ghana, Septemba 16, 2025. (Kundi la Kampuni za Greenhouse International Development nchini Ghana/kupitia Xinhua)
ACCRA - Jumuiya za Wachina nchini Ghana zimetoa msaada wa mahitaji wenye thamani ya Cedi zaidi ya milioni 2 (karibu Dola za Kimarekani 163,000) kwa waathiriwa wa mgogoro wa vurugu za hivi karibuni katika Mkoa wa Savannah nchini humo.
Kwa mujibu wa Kundi la Kampuni za Greenhouse International Development na Jumuiya ya Jamii za Wachina wa Ghana, vitu vinavyotolewa nao ni pamoja na mchele, vinywaji baridi, nyanya nzito, mablanketi, ndoo, koili za dawa za mbu, sabuni za kufulia na za usafi, na pedi za usafi.
Kampuni hiyo imeeleza kuwa, mahitaji hayo yaliwasili katika wilaya zilizoathirika siku ya Jumanne na Ijumaa wiki iliyopita.
Waziri wa Mkoa wa Savannah Salisu Be-Awuribe amezipongeza jumuiya za Wachina kwa msaada wao. "Kwa niaba ya watu wa Savannah na Rais wa Ghana, nataka kusema asante sana. Vitu vya mahitaji vitagawiwa kwa wale wanaovihitaji zaidi," waziri huyo amesema.
Mapigano hayo makali kati ya makabila ya Wabrifo na Wagonja mwishoni mwa Agosti juu ya ardhi inayozozaniwa yalisababisha vifo vya watu 31, watu kadhaa kujeruhiwa, na wengi kulazimika kuyahama makazi yao, huku mashamba, masoko na biashara vikiachwa au kuharibiwa.

Mfanyakazi akipakia msaada wa mahitaji uliotolewa na jumuiya za Wachina nchini Ghana mjini Accra, Ghana, Septemba 17, 2025. (Kundi la Kampuni za Greenhouse International Development nchini Ghana/kupitia Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Septemba 13, 2025 ikionyesha malori mawili yaliyopakiwa msaada wa mahitaji uliotolewa na jumuiya za Wachina nchini Ghana mjini Accra, Ghana. (Kundi la Kampuni za Greenhouse International Development nchini Ghana/kupitia Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



