Rais Xi Jinping atuma salamu kabla ya sikukuu ya mavuno ya wakulima wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 23, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC ametuma salamu za sikukuu ya mavuno kwa wakulima na watu wanaofanya kazi katika mstari wa mbele wa kilimo, vijiji na mambo ya wakulima kabla ya sikukuu ya nane ya mavuno ya wakulima wa China.

Amesisitiza juhudi za kujenga vijiji viwe vya kupendeza na vyenye hali ya mapatano ambayo yanafaa kwa watu kuishi na kufanya kazi, na kusonga mbele kwa pamoja kuelekea mustakabali mzuri wa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Rais Xi amesema ingawa imekumbwa na athari za ukame na mafuriko, China imeweza kupata mavuno tulivu ya nafaka ya majira ya joto na kuongeza uzalishaji wa mpunga wa mapema mwaka huu, na inatarajia kukaribisha tena mwaka wa mavuno. "Kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, ni lazima kufikia mambo ya kisasa katika kilimo na vijiji," Rais Xi amesema.

Rais Xi amesema ni muhimu kutoa kipaumbele cha juu kwa maendeleo ya kilimo na vijiji, kukamilisha sera zinazohusu kuimarisha kilimo, kunufaisha wakulima, na kuleta ustawi kwa vijiji, kuunga mkono maendeleo ya sayansi na teknolojia za kilimo, na zana na vifaa, na kufanya juhudi za kuinua uwezo wa jumla wa uzalishaji wa kilimo.

Ametoa wito wa kuchukua hatua mbalimbali za kuongeza nafasi za ajira na mapato kwa wakulima, na kusukuma mbele maendeleo halisi ya ustawishaji wa pande zote wa vijijini.

Sikukuu ya mavuno ya wakulima wa China ni sikukuu ya kwanza ya kitaifa iliyoanzishwa mahsusi kwa ajili ya wakulima wa China. Ikiwa ilianza rasmi mwaka 2018, sikukuu hiyo hutokea wakati sawa na Kipindi cha Mlingano wa Usiku na Mchana cha Majira ya Mpukutiko kila mwaka, ambacho ni moja ya vipindi 24 vya kalenda ya Kilimo ya China na kwa kawaida huwadia kati ya Septemba 22 na 24 wakati wa majira ya mavuno ya kilimo nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha