Lugha Nyingine
China kufanya mkutano wa kilele wa kimataifa wa wanawake mjini Beijing
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Guo Jiakun ametangaza Jumatatu kuwa China itafanya mkutano wa kilele wa wanawake duniani hivi karibuni mjini Beijing ili kuadhimisha miaka 30 tangu kufanyika Mkutano wa Wanawake wa Kimataifa wa mwaka 1995.
Guo amesema hayo kwenye mkutano na wanahabari, wakati alipoulizwa kufafanua zaidi juu ya waraka, wenye kichwa "Mafanikio ya China Ya Pande Zote Kwenye Maendeleo ya Wanawake katika Zama Mpya," uliotolewa Ijumaa mwishoni mwa wiki iliyopita na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China.
Ameongeza kuwa kutolewa kwa waraka huo kunalenga kuonesha kikamilifu mafanikio muhimu ya China katika kutekeleza Azimio la Beijing na Jukwaa la Kuchukua Hatua, kuwasilisha kwa utaratibu dhana, kanuni na shughuli za kibunifu za kuhimiza usawa wa kijinsia na maendeleo ya pande zote ya wanawake katika zama mpya, na kuchangia busara na uzoefu wa China kwenye harakati za maendeleo ya wanawake duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



