Mkutano wa kimataifa wa uhifadhi wa viumbe duniani wafanyika China kwa mara ya kwanza

(CRI Online) Septemba 23, 2025

Mkutano wa tano wa kimataifa wa uhifadhi wa viumbe umefunguliwa jana Jumatatu Septemba 22 mjini Hangzhou mkoani Zhejiang, China, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kufanyika barani Asia huku ukiwa na ushiriki mpana zaidi wa pande wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)

Katibu Mkuu wa Mpango wa Uhusiano kati ya Binadamu na Mfumo wa Mazingira ya Viumbe (MAB) wa UNESCO, Bw. Antonio Abreu, amesema, hifadhi za viumbe za China zimezidi kuonesha maono ya binadamu kuweza kuishi na kustawi pamoja na mazingira ya asili, huku zikipata uzoefu mkubwa katika matumizi ya teknolojia za hali ya juu ikiwemo teknolojia ya kidijitali.

Amesema kuwa, uzoefu huo wa China unastahili kuigwa kwenye jamii ya kimataifa.

Mkutano huo utajadili na kupitisha Mpango wa Binadamu na Mfumo wa Viumbe na Mpango Mkakati Tendaji wa Hangzhou wa Mtandao wa Hifadhi za Viumbea Duniani wa UNESCO, kutoa Azimio la Hangzhou, kuweka mpango wa maendeleo kwa miaka kumi ijayo, na kutoa suluhu za China kwa usimamizi wa ikolojia ya viumbe duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha