Kampuni ya uendeshaji wa reli ya SGR ya Kenya yazindua programu ya mafunzo ili kuboresha ujuzi wa wafanyakazi wazawa

(CRI Online) Septemba 23, 2025

Kampuni ya Afristar inayoendesha Reli ya Standard Gauge (SGR) ya Kenya iliyojengwa na kampuni ya China, imeanzisha programu ya mafunzo ya miezi sita yanayotolewa na maprofesa kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Reli cha Guangzhou, China ili kusaidia kuboresha ujuzi wa kiufundi kwa wafanyakazi wenyeji.

Kampuni hiyo imesema kwenye taarifa yake iliyotolewa jana Jumatatu kwamba mafunzo hayo, yanayofanyika mjini Nairobi, yanafanyika chini ya msingi wa uhusiano wa muda mrefu na taasisi za China, na katika mkakati wake mkuu wa uhamishaji ujuzi kwa wenyeji.

Tangu reli hiyo ya SGR ianze kufanya kazi tarehe 31 Mei, 2017, katika kipande Mombasa-Nairobi, hadi sasa zaidi ya wafanyakazi 3,500 wa Kenya wamepata mafunzo ya juu katika taasisi kubwa za taaluma ya reli za China, kikiwemo Chuo Kikuu cha Jiaotong cha Kusini Magharibi na Chuo cha Ufundi wa Reli cha Baoji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha