Mkutano wa kemikali za kilimo wa China na Afrika wafunguliwa Nairobi ili kuhimiza usalama wa chakula

(CRI Online) Septemba 23, 2025

Mkutano wa saba wa kilele wa kemikali za kilimo kati ya China na Afrika (CAC), ambao ni jukwaa la biashara kwa sekta ya kemikali za kilimo duniani, umefunguliwa jana Jumatatu mjini Nairobi, ukiangazia kuhimiza usalama wa chakula katika kanda hiyo.

Mkutano huo wa siku mbili, ulioandaliwa na Shirika la Sekta ya Kemikali lililo chini ya Kamati ya China ya Kuhimiza Biashara ya Kimataifa (CCPIT), Bodi ya Bidhaa za Kudhibiti Wadudu ya Kenya (PCPB) na Chuo Kikuu cha Egerton cha Kenya, unawakutanisha waoneshaji bidhaa wapatao 30, wengi wao wakiwa kutoka China, na kuonesha pembejeo bora, vifaa vya kilimo na suluhisho la kuongeza tija katika sekta ya kilimo.

Konsela wa Ubalozi wa China nchini Kenya, Zhu Li, amesema mkutano huo umetoa fursa muhimu ya kuimarisha maelewano, kuchangia uzoefu bora na kupanua wigo wa ushirikiano.

Ameongeza kuwa utoaji wa dawa za kilimo zenye ubora wa juu kutoka China umechukua nafasi muhimu katika kuhimiza sekta ya kilimo ya Kenya kupitia kusaidia wakulima kulinda mazao, kuongeza uzalishaji na kuimarisha usalama wa chakula.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha