Lugha Nyingine
Sudan Kusini yaanza kampeni ya afya kulinda watu zaidi ya milioni 3 dhidi ya magonjwa
Sudan Kusini kwa kushirikiana na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa (UN), imezindua kampeni ya afya kulinda watoto zaidi ya milioni 2.1 na watu wazima milioni 1.2 dhidi ya Polio na kichocho, magonjwa yanayoweza kuleta ulemavu.
Kampeni hiyo itafanyika kwa siku nne ambapo wafanyakazi wa afya na watu wa kujitolea wataenda nyumba hadi nyumba katika wilaya 40 kutoa chanjo dhidi ya Polio ya matone kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano, na vidonge vya Praziquantel kwa watoto wa shule na jamii zinazokumbwa na hatari ya kichocho katika wilaya tatu.
Waziri wa Afya wa Sudan Kusini Bibi Sarah Cleto Rial amesema mkakati huo wa pamoja unaotekelezwa kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa unalenga kuondoa changamoto za kufikia watu katika maeneo ambayo ni vigumu kufikika, na kuboresha kiwango cha chanjo ili kuzuia milipuko ya virusi vya Polio aina ya 2, ambavyo vimeongezeka kutokana na utoaji mdogo wa chanjo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



