WHO yahimiza nchi za Afrika kupanua upatikanaji wa huduma shufaa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 24, 2025

Lawrence Ookeditse, kaimu waziri wa afya wa Botswana, akizungumza kwenye Mkutano wa 5 wa Mawaziri wa Afya wa Afrika kuhusu Huduma Shufaa, uliofanyika kama sehemu ya Mkutano wa 8 wa Kimataifa wa Huduma Shufaa na Huduma Shirikishi wa Afrika, mjini Gaborone, Botswana, Septemba 23, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE - Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito kwa nchi za Afrika kuweka kipaumbele katika kujumuisha huduma shufaa kwenye mifumo yao ya afya ya kitaifa, ambazo ni huduma zinazolenga kuwapa ahueni wagonjwa, kuzifanya zipatikane kwa wote, zenye kufikika, na za bei nafuu kwa watu wote katika bara hilo.

Fabian Ndenzako, mwakilishi wa WHO nchini Botswana na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, ametoa wito huo kwenye Mkutano wa 5 wa Mawaziri wa Afya wa Afrika kuhusu Huduma Shufaa, unaofanyika kama sehemu ya Mkutano wa 8 wa Kimataifa wa Huduma Shufaa na Huduma Shirikishi wa Afrika ambao umeanza jana Jumanne na utaendelea hadi Ijumaa mjini Gaborone, mji mkuu wa Botswana.

Ndenzako amesisitiza kuwa Afrika inaendelea kubeba mzigo mkubwa wa magonjwa yanayotishia maisha huku ikikabiliwa na vizuizi vikubwa vya kisheria na usambazaji katika kufikia na kupata dawa muhimu za kutuliza maumivu.

Amepongeza hatua iliyofikiwa na serikali nyingi katika bara hilo. "Serikali nyingi zimejumuisha huduma shufaa katika nyaraka, mikakati na miongozo yao ya huduma ya afya kwa wote," amesema, pia akiongeza kuwa maendeleo katika kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya na kuunga mkono mifano bora ya huduma zenye msingi wa kijamii na za nyumbani.

Lawrence Ookeditse, kaimu waziri wa afya wa Botswana, amepongeza hatua za nchi hiyo, kama vile kuzinduliwa kwa Sera yake ya Taifa ya Huduma za Tiba za Nyumbani na Shufaa. Hata hivyo, amerejelea changamoto zinazoendelea, zikiwemo za kuiweka siasa kuwa kipaumbele, upatikanaji fedha, ufikiaji na upatikanaji wa vifaa.

Ookeditse amesisitiza dhamira ya serikali katika kuimarisha vyote huduma za nyumbani za jamii na huduma shufaa.

"Kwa pamoja tutatetea uungaji mkono imara zaidi, kiwango cha juu cha uwekezaji, na sera bora ambazo zinatanguliza mahitaji ya watu wetu walio mazingira hatarishi zaidi," amesema.

Lawrence Ookeditse, kaimu waziri wa afya wa Botswana, akizungumza kwenye Mkutano wa 5 wa Mawaziri wa Afya wa Afrika kuhusu Huduma Shufaa, uliofanyika kama sehemu ya Mkutano wa 8 wa Kimataifa wa Huduma Shufaa na Huduma Shirikishi wa Afrika, mjini Gaborone, Botswana, Septemba 23, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Lawrence Ookeditse, kaimu waziri wa afya wa Botswana, akizungumza kwenye Mkutano wa 5 wa Mawaziri wa Afya wa Afrika kuhusu Huduma Shufaa, uliofanyika kama sehemu ya Mkutano wa 8 wa Kimataifa wa Huduma Shufaa na Huduma Shirikishi wa Afrika, mjini Gaborone, Botswana, Septemba 23, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha