

Lugha Nyingine
Rais Xi atangaza Mchango wa Kitaifa wa Kukabili Mabadiliko ya Tabianchi wa 2035 wa China
Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba kwa njia ya video kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi 2025 uliofanyika New York, Septemba 24, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametoa hotuba yake kwa njia ya video kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Tabianchi uliofanyika New York, Marekani jana Jumatano kwa saa za huko akisema kwamba mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 10 tangu kusainiwa kwa Makubaliano ya Paris, na pia ni mwaka muhimu kwa nchi mbalimbali duniani kuwasilisha Mchango wa Kitaifa wa Kukabili Mabadiliko ya Tabianchi (NDCs) na vitendo vya kukabiliana na Tabianchi duniani vinaingia katika kipindi muhimu.
Ametoa mapendekezo matatu yafuatayo:
Kwanza, Rais Xi amesema ni muhimu kuimarisha imani. "Mpito kuelekea kijani na utoaji kaboni chache ni wimbi la zama zetu. Wakati baadhi ya nchi zinafanya kinyume chake, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuendelea kudumisha mwelekeo sahihi, kuwa na imani thabiti, na kutotelekeza vitendo na kuchukua hatua halisi za kudumu, kusukuma mbele utungaji na utekelezaji wa NDCs, ili kutoa nguvu chanya zaidi kwa ushirikiano katika usimamizi wa Tabianchi duniani," amesema.
Pili, Rais Xi ametoa wito wa kubeba wajibu. "Lazima kulinda Haki na usawa, na kuheshimu vya kutosha haki ya maendeleo ya nchi zinazoendelea," amesema.
"Mpito wa kijani duniani unapaswa kupunguzwa, badala yake kupanua pengo kati ya Nchi za Kaskazini na Nchi za Kusini. Nchi mbalimbali zinahitaji kuheshimu kanuni ya wajibu wa pamoja lakini ni wenye tofauti, ambapo nchi zilizoendelea zinapaswa kufanya kazi ya kuongoza katika kutimiza wajibu wa kupunguza utoaji hewa chafuzi na kutoa uungaji mkono zaidi wa kifedha na kiteknolojia kwa nchi zinazoendelea," ameongeza.
Tatu, Rais Xi amesisitiza umuhimu wa kuzidisha ushirikiano, akiongeza kuwa uratibu wa kimataifa katika teknolojia na viwanda vya kijani unapaswa kuimarishwa ili kukabiliana na mapungufu katika uwezo wa uzalishaji wa kijani na kuhakikisha mzunguko huria wa bidhaa bora za kijani duniani, na kuyawezesha manufaa ya maendeleo ya kijani yafikie pembe zote za dunia.
Rais Xi ametangaza NDCs ya China kama ifuatavyo: Ifikapo mwaka 2035, China itapunguza utoaji wa hewa chafuzi katika uchumi mzima kwa asilimia 7 hadi asilimia 10 kutoka viwango vya kilele, ikijitahidi kufanya vizuri zaidi; kuongeza sehemu ya mafuta yasiyo ya kisukuku katika matumizi ya jumla ya nishati hadi asilimia zaidi ya 30; kupanua uwezo wa jumla wa mashine za utoaji nishati zinazotokana na upepo na jua hadi zaidi ya mara sita ya viwango vya 2020, ikijitahidi kufikisha jumla ya gigawati 3,600.
Aidha, amesema China itaongeza jumla ya uhifadhi wa misitu hadi mita za ujazo zaidi ya bilioni 24; kufanya magari yanayotumia nishati mpya kuwa mengi zaidi katika mauzo ya magari mapya; kupanua Soko la Kitaifa la Biashara ya Utoaji Kaboni kufikia sekta kuu zinazotoa hewa chafuzi kwa wingi; na kimsingi kuanzisha jamii inayoweza kuhimili Tabianchi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma