

Lugha Nyingine
Rais Xi ahudhuria tamasha la usiku la kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa Mkoa wa Xinjiang wa China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akipungia mkono watu wakati akihudhuria tamasha la usiku la kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang mjini Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo, Septemba 24, 2025. (Xinhua/Shen Hong)
URUMQ - Rais wa China Xi Jinping amehudhuria tamasha la usiku la kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang mjini Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo, jana Jumatano jioni ambapo akitazama maonesho ya tamasha hilo la "Xinjiang ya Kupendeza" pamoja na watu wa makabila mbalimbali mkoani humo.
Tamasha hilo la usiku lilikuwa na maonesho ya michezo ya sanaa ya sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ilionesha juhudi kubwa katika ujenzi wa kijamaa wa Xinjiang. Sehemu ya pili ilionesha ustawi ulioletwa na mageuzi na ufunguaji mlango katika mkoa huo, na sehemu ya mwisho ilionyesha matarajio mazuri ya watu wa makabila mbalimbali ya Xinjiang wakifanya kazi pamoja kufikia ndoto zao katika zama mpya.
Viongozi waandamizi, akiwemo Wang Huning na Cai Qi, pia walitazama tamasha hilo.
Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), aliwasili Urumqi juzi Jumanne kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za maadhimisho.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akipungia mkono watu wakati akihudhuria tamasha la usiku la kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang mjini Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo, Septemba 24, 2025. (Xinhua/Ding Lin)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akipungia mkono watu wakati akihudhuria tamasha la usiku la kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang mjini Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo, Septemba 24, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma