

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping wa China asisitiza kujenga Xinjiang ya mambo ya kisasa ya kijamaa
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu baada ya kusikiliza ripoti za kazi kutoka kamati ya Chama na serikali ya mkoa huko Urumqi, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, Septemba 24, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
URUMQI - Rais wa China Xi Jinping ameuhimiza Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China kujenga Xinjiang mpya ya mambo ya kisasa ya kijamaa yenye sifa ya mshikamano, maelewano, ustawi, utajiri, mambo ya utamaduni yanayoendelea, na mazingira mazuri ya kiikolojia, ambapo watu wanaishi na kufanya kazi kwa amani na kuridhika.
Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameyasema hayo baada ya kusikiliza ripoti za kazi kutoka kamati ya Chama na serikali ya mkoa huo jana Jumatano.
Amesisitiza kutekeleza sera na hatua za Chama kwa pande zote, kwa kutii na kwa kina, na kutoa miongozo kwa ajili ya maendeleo ya Xinjiang ya zama mpya. Rais Xi amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Mkoa huo miaka 70 iliyopita, mabadiliko makubwa sana yamekuwa yakitokea katika mkoa huo, na Xinjiang imeanza safari mpya pamoja na sehemu nyingine nchini China katika kujenga nchi ya mambo ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote.
Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa Pato la Jumla la Xinjiang limekuwa likikua kwa wastani wa asilimia 7.04 kwa mwaka tangu 2012. Mwaka 2024, liliongezeka kwa asilimia 6.1, likipita yuan trilioni 2 (dola za Kimarekani karibu bilioni 281.4) kwa mara ya kwanza.
"Kwa kutumia vya kutosha rasilimali zake na uwezo wa viwanda vyake, Xinjiang inapaswa kufanya juhudi za kutafuta njia ya maendeleo ya sifa bora inayofaa hali yake yenyewe na kukuza nguvu zake mpya za uzalishaji zenye sifa bora kutokana na mazingira yake ya ndani," Rais Xi amesisitiza.
Pia ameihimiza Xinjiang kuhimiza sekta ya utalii wa kitamaduni, kuimarisha uhifadhi na urejeshaji mifumo ya ikolojia, kuharakisha ujenzi wa eneo la msingi kwenye Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri, na kutoa kipaumbele katika kuhakikisha na kuboresha hali ya maisha ya watu.
Rais Xi amesisitiza juhudi za kila upande katika kudumisha utulivu wa jamii mkoani Xinjiang, na kuongeza uelewa na utayari wa watu kuhusu kupambana na ugaidi na kudumisha utulivu.
"Ni muhimu kujenga uelewa zaidi juu ya taifa la China kama jumuiya moja mkoani Xinjiang na kuhimiza ujenzi wa jumuiya," Rais Xi amesema, akiongeza kuwa mkoa huo unapaswa kufanya jitihada za kuhakikisha kwamba dini nchini China zinalingana na hali halisi ilivyo ya China , na kusaidia makada na watu wa makabila mbalimbali kujenga utambuzi sahihi juu ya nchi, historia, taifa, utamaduni na dini.
Rais Xi, akiongoza ujumbe wa Kamati kuu ya Chama na serikali kuu aliwasili Urumqi, mji mkuu wa Xinjiang juzi Jumanne kushiriki kwenye shughuli za kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa mkoa huo unaojiendesha.
Jana Jumatano asubuhi, Rais Xi alitembelea maonyesho yenye mambo ya maadhimisho hayo kwenye kituo cha kitamaduni mjini Urumqi. Pia atashiriki kwenye mkusanyiko mkubwa wa sherehe mjini humo leo Alhamisi.
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu baada ya kusikiliza ripoti za kazi kutoka kamati ya Chama na serikali ya mkoa wa Xinjiang huko Urumqi, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, Septemba 24, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu baada ya kusikiliza ripoti za kazi kutoka kamati ya Chama na serikali ya mkoa wa Xinjiang huko Urumqi, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, Septemba 24, 2025. (Xinhua/Ding Lin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma