Lugha Nyingine
Maonyesho ya biashara ya China na Afrika Kusini yafunguliwa mjini Johannesburg
Mkutano wa Kutangaza Biashara na Uwekezaji kati ya Afrika Kusini na China na Maonesho ya tisa ya Biashara kati ya China na Afrika Kusini yamefunguliwa Jumanne wiki hii mjini Johannesburg, na kuvutia maelfu ya washiriki wanaotaka kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji.
Akihutubia hafla ya ufunguzi, Naibu waziri wa biashara, viwanda na ushindani wa Afrika Kusini Zuko Godlimpi, amebainisha kuwa biashara kati ya nchi hizo mbili inakua kwa kasi, na kuelezea uhusiano wa Afrika Kusini na China kama mfano muhimu wa ushirikiano wa Kusini-Kusini unaozingatia ushirikiano wa kimkakati.
Balozi wa China nchini Afrika Kusini Wu Peng amesema mkutano huo unalenga kutumia fursa zinazotokana na kuinuka kwa uhusiano wa nchi hizo mbili, akisisitiza kuwa ujuzi na uhamishaji wa teknolojia vilivyosisitizwa kwenye mkutano huo vitasaidia kuendeleza malengo ya maendeleo ya Afrika Kusini.
Maonyesho hayo ya siku tatu ya biashara, yatakayofikia tamati leo Alhamisi, yanashirikisha kampuni zaidi ya 500 za China zikionyesha bidhaa mbalimbali, zikiwemo chakula, vifaa, nguo, bidhaa za kilimo na bidhaa za matumizi ya nyumbani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



