Lugha Nyingine
Tume ya uchaguzi ya Uganda yamteua Museveni kuwa mgombea wa urais mwaka 2026
Tume ya Uchaguzi ya Uganda (EC) imemteua na kumtangaza rasmi Rais Yoweri Museveni kuwa mgombeaji wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2026 baada ya kuthibitisha fomu yake ya uteuzi katika makao makuu yake mjini Kampala.
Mwenyekiti wa EC Simon Mugenyi Byabakama amesema kuwa tume inatoa wito kwa washiriki wote, mawakala wao, wafuasi, na umma kwa ujumla kushikilia thamani ya amani, utu, na kuheshimiana wakati wote wa mchakato wa uteuzi na zaidi katika kipindi kijacho cha kampeni za wagombea urais.
Rais Museveni ameishukuru tume hiyo kwa kumteua na kumuidhinisha kugombea kwake. Amesema vipaumbele vyake vitajumuisha programu za uzalishaji mali, elimu bila malipo katika shule za serikali, matengenezo ya barabara, uboreshaji wa huduma za afya, na kukabiliana na uhalifu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



