China yarekodi safari za abiria za mara bilioni 2.4 za kuvuka mikoa katika kipindi cha kilele cha usafiri (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 10, 2025
China yarekodi safari za abiria za mara bilioni 2.4 za kuvuka mikoa katika kipindi cha kilele cha usafiri
Abiria wakionekana kwenye Stesheni ya Reli ya Mji Wuxi, katika Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Oktoba 7, 2025. (Picha na Huan Yueliang/Xinhua)

BEIJING - Katika siku nane za mapumziko wakati wa Sikukuu ya Taifa na Sikukuu ya Mbalamwezi ya Katikati mwa Majira ya Mpukutiko iliyomalizika Jumatano wiki hii nchini China, safari za abiria za kuvuka mikoa zilifikia mara takriban bilioni 2.43 kote nchini China, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ya China imetangaza jana Alhamisi.

Imesema kuwa, kuanzia Oktoba 1 hadi 8, wastani wa kila siku wa usafiri wa abiria ulifikia mara milioni 304 za kuvuka mikoa, zikiongezeka kwa asilimia 6.3 kuliko mwaka jana na kufikia rekodi ya juu.

Mahitaji ya machaguo ya usafiri kama vile safari za watalii wa vikundi vidogo, safari za watu kuendesha magari binafsi na safari za familia na za marafiki yaliendelea kuwa yenye nguvu, ikionesha vilivyo wimbi la usafiri la kipindi cha siku za mapumziko, wizara hiyo imesema.

Imesema, shirika la reli la China lilihudumia usafiri wa abiria mara milioni 153.96, na wastani wa kila siku ulifikia mara milioni 19.24, ukiongezeka kwa asilimia 2.6 kuliko mwaka uliopita, wizara hiyo imeeleza.

Wizara hiyo imesema kuwa, idadi ya abiria katika usafiri wa njia ya maji na usafiri wa anga ilifikia mara milioni 11.66 na mara milioni 19.14 mtawalia. Idadi ya abiria kwenye usafiri wa barabarani ilifikia mara bilioni 2.25, na wastani wa kila siku ulifikia mara milioni 281.05, na kuongezeka kwa asilimia 6.6 kuliko mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha