Njia ya moja kwa moja ya kusafirisha makontena kwa meli yaunganisha Miji ya Qingdao, China na Jeju, Korea Kusini (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 17, 2025
Njia ya moja kwa moja ya kusafirisha makontena kwa meli yaunganisha Miji ya Qingdao, China na Jeju, Korea Kusini
Hafla ya uzinduzi wa njia ya kusafirisha makontena kwa meli ya Qingdao-Jeju ikifanyika kwenye Gati la Usafiri wa Meli wa Kimataifa la Qingdao katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Oktoba 16, 2025. (Xinhua/Li Ziheng)

QINGDAO - Njia ya moja kwa moja yenye ratiba ya kudumu ya kusafirisha makontena kwa meli kati ya Mji wa Qingdao wa China na Mji wa Jeju wa Korea Kusini imezinduliwa rasmi jana Alhamisi ambapo njia hiyo ya usafirishaji wa haraka itafanya usafiri wa mara moja kwa wiki katika kipindi chake cha mwanzo, ikiongeza kwa kiasi kikubwa uchukuzi wa mizigo kati ya miji hiyo miwili.

Njia hiyo pia inatarajiwa kupunguza kwa ufanisi gharama za uchukuzi, na kuongeza zaidi vituo vya uchukuzi wa mzigo kwenye mtandao wa usafirishaji kwa meli wa Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China hadi Korea Kusini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha