Tamasha la sanaa la Njia ya Hariri lafunguliwa katika Mji wa Xi'an, Kaskazini Magharibi mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 20, 2025
Tamasha la sanaa la Njia ya Hariri lafunguliwa katika Mji wa Xi'an, Kaskazini Magharibi mwa China
Watembeleaji wakitazama kazi za sanaa kwenye Tamasha la 11 la Kimataifa la Sanaa la Njia ya Hariri kwenye Jumba la Makumbusho ya Sanaa la Mkoa wa Shaanxi mjini Xi'an, katika Mkoa wa Shaanxi, kaskazini-magharibi mwa China, Oktoba 19, 2025. (Xinhua/Zou Jingyi)

XI'AN - Tamasha la 11 la Kimataifa la Sanaa la Njia ya Hariri limefunguliwa mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini-magharibi mwa China, huku washiriki kutoka nchi na maeneo zaidi ya 80 wakiwasili kwa ajili ya shughuli ya siku 25 ya maonyesho mbalimbali ya sanaa.

Likiwa na kaulimbiu ya "Kuunganishwa kwa Njia ya Hariri, Kuungana Kupitia Sanaa," tamasha hilo la mwaka huu lililofunguliwa rasmi Alhamisi wiki iliyopita, limehusisha hafla za kufunguliwa na kufungwa, maonyesho ya jukwaani, miradi ya mawasiliano ya kitamaduni na maonyesho ya sanaa ya mwaliko wa kimataifa.

Jumla ya maonyesho 46 ya michezo ya sanaa jukwaani yatafanyika, ambayo mengi yao yatafanyika katika vyuo vikuu, maeneo ya makazi na maeneo ya biashara ili kuifanya kueneza zaidi sanaa.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2014, tamasha hilo limeshakaribisha washiriki kutoka nchi na maeneo zaidi ya 120 duniani. Hadi sasa, limeonyesha kazi za sanaa zaidi ya 4,500 na kuandaa maonyesho ya jukwaani zaidi ya 300 yaliyoshirikisha wasanii karibu 7,200, yakiimarisha uhusiano wa kitamaduni kati ya China na nchi nyingine duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha