Eneo la Genge la Longyang nchini China laendeleza uvuvi wa samaki wa silva na shughuli za utalii

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 21, 2025
Eneo la Genge la Longyang nchini China laendeleza uvuvi wa samaki wa silva na shughuli za utalii
Mfanyakazi akichambua samaki wa silva waliovunwa punde kwenye eneo la Genge la Longyang katika Wilaya ya Gonghe ya Eneo linalojiendesha la kabila la Watibeti la Hainan katika Mkoa wa Qinghai, kaskazini-magharibi mwa China, Oktoba 18, 2025. (Xinhua/Qi Zhiyue)

Kila mwaka kuanzia mwishoni mwa Agosti hadi mwishoni mwa Novemba, wavuvi kwenye eneo la Genge la Longyang katika Mkoa wa Qinghai, kaskazini-magharibi mwa China wanakuwa na pilika nyingi za kuvuna samaki wa silva.

Katika miaka ya hivi karibuni, eneo hilo la Genge la Longyang limekuwa likitumia vya kutosha maliasili zake nyingi za maji na mazingira mazuri ya kiikolojia kuendeleza kazi ya uvuvi ya samaki wa silva na shughuli za utalii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha