Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao la China lashughulikia safari za abiria zaidi ya milioni 93 katika miaka saba iliyopita (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 23, 2025
Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao la China lashughulikia safari za abiria zaidi ya milioni 93 katika miaka saba iliyopita
Picha ya iliyopigwa Oktoba 19, 2025 ikionyesha meli za kitalii zikipita chini ya Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao kusini mwa China. (Xinhua/Deng Hua)

GUANGZHOU - Safari zaidi ya milioni 93.34 za abiria wanaoingia na kutoka zilikuwa zimerekodiwa kupitia bandari ya Zhuhai ya Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao hadi kufikia jana Jumatano, miaka saba baada ya daraja hilo kufunguliwa rasmi kwa matumizi.

Kituo cha ukaguzi wa mpaka wa daraja hilo kinasema, kilishughulikia safari za abiria milioni 12.88 na safari za magari 860,000 mwaka 2019. Takwimu hizo zimepanda hadi milioni 27 na milioni 5.55, mtawalia, mwaka 2024, na zimezidi milioni 25.1 na milioni 5.46, mtawalia, hadi sasa mwaka huu, zikiwa na ongezeko la asilimia 17 na 25, mtawalia, zikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

"Kutokana na kuendelea kuongezeka kwa abiria na magari bandarini, inatarajiwa kuwa mwaka 2025 jumla ya safari za abiria kupitia bandari zitazidi milioni 30 na jumla ya magari itakuwa zaidi ya milioni 6," amesema Chen Faqiu, mkuu wa kituo hicho cha ukaguzi.

Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 55 linalounganisha Mikoa ya Utawala Maalum ya Hong Kong na Macao na Mji wa Zhuhai, yote ikiwa kusini mwa China, lilifunguliwa kwa matumizi mwaka Oktoba 23, 2018. Ni barabara kuu ya kivuko cha daraja na handaki la kupita chini maji baharini chenye refu zaidi duniani.

Upanuzi wa utalii wa watu binafsi kutoka China Bara hadi Hong Kong na Macao umestawisha shughuli za utalii kwa kiasi kikubwa kupitia daraja hilo. Takwimu kutoka kituo hicho cha ukaguzi zinaonyesha kuwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kituo hicho kimehudumia watalii zaidi ya milioni 10.15 kutoka China Bara, ikiweka rekodi, huku idadi hiyo ikijumuisha wageni milioni 4.6 wenye viza za kitalii.

Wakati huo huo, daraja hilo limefupisha muda wa kuendesha gari kutoka Hong Kong hadi Zhuhai na Macao kutoka saa tatu hadi dakika takribani 45. Mwaka 2023, bandari hiyo ya Zhuhai ilishuhudia magari takriban 9,000 kupita kila siku, ambao umeongezeka hadi kufikia zaidi ya 18,000 kwa sasa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha