Lugha Nyingine
Maonyesho ya Canton yavutia idadi ya wanunuzi duniani ya kuweka rekodi (3)
GUANGZHOU - Awamu ya pili ya Maonyesho ya 138 ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya China, ambayo pia yanafahamika kwa jina la Maonyesho ya Canton imefunguliwa jana Alhamisi katika Mji wa Guangzhou, kusini mwa China, ikihusisha bidhaa bora za matumizi ya nyumbani.
Mwandaaji wa maonyesho hayo alisema, awamu mbili za maonyesho hayo zimevutia wanunuzi zaidi ya 157,000 wa ng'ambo kutoka nchi na maeneo 222, ikifikia kiwango cha juu katika historia na ongezeko la asilimia 6.3 kutoka maonyesho yaliyopita.
Ikionesha zaidi vitu vya matumizi ya nyumbani, zawadi, mapambo, vifaa vya ujenzi, na samani, awamu hiyo ya pili ya maonyesho inashirikisha kampuni zaidi ya 10,000 zinazoonesha bidhaa.
Wanunuzi wa kimataifa wamesifu maonyesho hayo wakiyaelezea kuwa yasiyo na mbadala kwa biashara ya kimataifa, wakielezea minyororo himilivu ya viwanda na usambazaji bidhaa ya China kuwa ni yenye kutuliza hali katika nyakati zenye misukosuko.
Mnunuzi kutoka Canada amesifu roboti na otomatiki za hali ya juu za China, huku mnunuzi kutoka Georgia akisisitiza thamani ya kuuziana na kuzungumza ana kwa ana baada ya kushiriki kwa mara ya 20.
Awamu hiyo ya pili ya maonyesho imevutia kampuni kubwa za kuuza kwa rejareja duniani 145, zikiwemo Target na Kingfisher, ikiashiria imani kubwa katika jukumu la China la kuwa kitovu kikuu cha viwanda.
Yakiwa yalianza kufanyika kuanzia Oktoba 15 na yamepangwa kuendelea hadi Novemba 4 katika awamu zake zote tatu, Maonyesho hayo ya 138 ya Canton yanajivunia rekodi ya kuwa na mabanda 74,600 na waonyeshaji bidhaa zaidi ya 32,000.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




