Meli kubwa zaidi ya kubeba mizigo ya China inayotumia umeme kwa mambo yote yazinduliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 24, 2025
Meli kubwa zaidi ya kubeba mizigo ya China inayotumia umeme kwa mambo yote yazinduliwa
Picha hii iliyopigwa Oktoba 23, 2025 ikionyesha meli ya kubeba mizigo ya Gezhouba inayotumia umeme kwa mambo yote mjini Yichang, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China. (Xinhua/Xiao Yijiu)

WUHAN - Meli kubwa zaidi ya kubeba mizigo ya China inayotumia umeme kwa mambo yote, iliyopewa jina la Gezhouba, imezinduliwa rasmi jana Alhamisi mjini Yichang, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, likiashiria hatua kubwa muhimu katika sekta ya usafirishaji wa meli wa kijani na wa teknolojia za kisasa ya nchi hiyo.

Meli hiyo, yenye urefu wa karibu mita 130 na uwezo wa kubeba mzigo wa tani zaidi ya 13,000, ina vifaa 12 vya betri za umeme za lithiamu zenye uwezo wa kutoa kwa jumla nishati ya kWh 24,000.

Muundaji wake amesema meli hiyo inaruhusu ubadilishaji wa betri kwa haraka na inajivunia kuendeshwa kwa umbali wa kilomita 500.

Kwa upande wa teknolojia ya kisasa, meli hiyo ina mfumo wa udhibiti ambao unawezesha urambazaji wa kutokea mbali na kutia nanga kiotomatiki, uliounganishwa na mitandao ya mawasiliano ya viunganishi mbalimbali.

Msomi kutoka Akademia ya Uhandisi ya China Yan Xinping amesisitiza kwamba mradi huo ni zaidi ya uvumbuzi wa bidhaa moja -- kwani unathibitisha mafanikio ya teknolojia muhimu kama vile betri zenye uwezo mkubwa na mifumo ya umeme ya DC inayosambazwa.

Meli hiyo ya kubeba mizigo inatarajiwa kuokoa tani takriban 617 za mafuta kwa mwaka na kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni dioksidi kwa mwaka kwa tani 2,052.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha