Jengo jipya la kinara la Eneo la Ghuba Kubwa la China launganishwa kwenye karibu mita 120 juu ya ardhi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2025

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Katika siku za karibuni, mradi wa ujenzi wa Mnara C wa Kituo cha Makao Makuu ya Shenzhen Bay Super, eneo maalumu la kiuchumi la mji wa Shenzhen, China, umekamilisha kazi ya kuunganisha ushoroba wake wa chuma yenye uzito wa tani 6,000 kwenye sehemu ya mita 119.15 juu ya ardhi, ukifikia usahihi wa kiwango cha milimita.

Mnara C una muundo wa minara pacha wenye urefu mkubwa sana, na ushoroba huo kwenye sehemu ndefu zaidi unafikia mita 78.

Kituo hicho na Hong Kong vipo pande mbili za ghuba ya Guangdong-Hong Kong-Macau, na baada ya kukamilisha kwa ujenzi wake, kituo hicho kitakuwa mnara mpya wa eneo la ghuba hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha