Mzee wa Zanzibar, Tanzania, apata fursa mpya ya uhai  kutokana na utaalamu wa matibabu ya madaktari wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2025

Madaktari wa China na Tanzania na mgonjwa Omar Haji Makame wakiwa pamoja baada ya upasuaji wa laparoscopic kufanikiwa katika Hospitali ya Lumumba katika Zanzibar, Tanzania, Oktoba 20, 2025. (Timu ya 35 ya madaktari wa China katika Zanzibar / Xinhua)

Madaktari wa China na Tanzania na mgonjwa Omar Haji Makame wakiwa pamoja baada ya upasuaji wa laparoscopic kufanikiwa katika Hospitali ya Lumumba katika Zanzibar, Tanzania, Oktoba 20, 2025. (Timu ya 35 ya madaktari wa China katika Zanzibar / Xinhua)

DAR ES SALAAM, – Kwa Omar Haji Makame, mzee wa Zanzibar mwenye umri wa miaka 74, ambaye ni mkazi mpole mwenye tabia ya kukaa kimyakimya, miezi mitano iliyopita imekuwa na muda uliojaa uchungu wa maumivu, na hali isiyo na uhakika hatimaye uliojaa matumaini mapya.

Mwanawe alisema, mwanzoni alisumbuliwa na tatizo la gesi tumboni , kisha maumivu makali ya tumbo yakamfanya Makame ashindwe kujisaidia na kuanza kutapika sana. Madaktari waligundua alikuwa na hali ya vizuizi ndani ya tumbo na uvimbe kwenye koloni ya sigmoid, na wakafanya upasuaji wa dharura wa colostomy ili kuokoa maisha yake.

Baada ya wiki kadhaa, uvimbe ulitokea karibu na stoma yake, uchunguzi wa hali hii umethibitishwa kuwa ni hernia ya parastomal. Baada ya kufanyiwa upasuaji mwingine na dura tatu za tiba kemikali, uvimbe bado ulikuwa na tatizo.

Haitham Hassan, daktari wa Hospitali ya Lumumba, alisema kuwa hali ya Makame ilizidi kuwa na utatanishi, alifikiri kufanya upasuaji wa kuondoa sehemu ya utumbo.

Wakati huo huo, Timu ya 35 ya madaktari wa China ilifika katika Hospitali ya Lumumba ya Zanzibar. Mmmoja miongoni mwa madaktari hao Bao Zengtao, daktari bingwa wa upasuaji wa jumla na kiongozi wa timu, ambaye hakusita kufanya kila juhudi kumuokoa Makame.

Daktari Bao, kwa kushirikiana na daktari Hassan, walifanya tathmini kamili ikiwemo kuongeza uchunguzi wa CT wa tumbo na kufanya vipimo vya alama za uvimbe. Bao alithibitisha kuwa Makame alikuwa anafaa kufanyiwa upasuaji wa kisasa wa laparoscopic wenye uingiliaji mdogo (minimally invasive).

Bao Zengtao (wa kwanza kushoto), daktari wa upasuaji na kiongozi wa timu ya 35 ya madaktari wa China katika Zanzibar, na madaktari wa Tanzania wakati wanapofanya upasuaji wa laparoscopic katika Hospitali ya Lumumba katika Zanzibar, Tanzania, Oktoba 20, 2025. (Timu ya 35 ya madaktari wa China Zanzibar / Xinhua)

Bao Zengtao (wa kwanza kushoto), daktari wa upasuaji na kiongozi wa timu ya 35 ya madaktari wa China katika Zanzibar, na madaktari wa Tanzania wakati wanapofanya upasuaji wa laparoscopic katika Hospitali ya Lumumba katika Zanzibar, Tanzania, Oktoba 20, 2025. (Timu ya 35 ya madaktari wa China Zanzibar / Xinhua)

Katika siku ya upasuaji, kikundi cha upasuaji chenye madaktari mbalimbali kiliundwa, ambapo Daktari Bao aliongoza upasuaji, akisaidiwa na daktari Hassan, daktari wa mkojo Wang Kunpeng, na daktari wa usingizi Luan Hengfei.

Madaktari hao walimaliza upasuaji wa laparoscopic wa kuondoa saratani ya koloni ya sigmoid, kufanya upasuaji wa kufunga stoma kuwa hali ya kawaida, na kutibu hernia ndani ya upasuaji huu mmoja. Hii ni mara ya kwanza kwa hospitali ya Zanzibar kufanya upasuaji kwa teknolojia hii ya kisasa.

“Sitavumilia tena na maumivu ya stoma. Naweza kuishi kama mtu wa kawaida,” alisema Makame kwa shukrani kwa timu ya madaktari.

Tangu miaka ya 1960, madaktari wa China zaidi ya 800 wamefanya kazi ya kutoa huduma za matibabu katika Zanzibar, wakifanya zaidi ya upasuaji 240,000 na kuokoa maisha ya maelfu ya watu.

Timu ya 35 ya madaktari wa China inaendeleza kazi hii, si kama tu walileta utaalamu wa matibabu, bali pia kutoa zana na vifaa muhimu na mafunzo ya matibabu. Mapema mwaka huu, Wizara ya Afya ya Zanzibar ilipokea zana na vifaa vya matibabu kutoka serikali ya China, ili kusaidia kazi ya upasuaji na kuzindua kambi za matibabu visiwani kote.

Makame anafungua ukurasa mpya wa maisha yake bila matatizo yaliyomsumbua. Hii inaonyesha kwamba, kila mafanikio ya upasuaji yanaleta mabadiliko ya maisha ya binadamu, na matibabu hayana mipaka.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha